Bondia Mnemwa aomba msaada wa matibabu aweze kurudi tena ulingoni

DAR-Bondia Mohammed Mnemwa ameomba msaada kwa Serikali, vyama vya mchezo wa ngumi pamoja na wadau kumsaidia kulipa gharama za matibabu anayopatiwa katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili.
Mnemwa alipatwa na matatizo ya kiafya baada ya kupigwa KO katika raundi ya tatu ya pambano alilocheza na Ally Sewe kwenye pambano lililofanyika Januari 24, 2025 katika ukumbi wa Mrina uliopo Manzese Tiptop jijini Dar es salaam.

Bondia Mnemwa amepeleka kilio chake kwa wadau ili apate msaada na aweze kupona ili kurudi tena ulingoni.

"Mimi kwa hali yangu nilikua naomba watu wajitokeze ikiwemo Serikali, vyama vya ngumi wanisaidie kwa gharama zitakazotajwa hapa ili niendelee kurudi kwenye michezo yangu kwa sababu ngumi ndio maisha yangu ambayo nimejichagulia.

"Kama misaada kama mtu yeyote mwenye uwezo watu wanaonijua waandaaji wa mapambano wasimamizi lazima wasogee kama kuja kuniona na watahusika na chochote kitu ili mwenyewe niweze kuinuka tena niendelee na shughuli zangu sasa hivi nasikia maumivu kwenye kichwa," amesema Mnemwa.

Bondia huyo kwa sasa anapatiwa matibabu kwenye taasisi ya mifupa MOI iliyopo chini ya Hospital ya Taifa ya Muhimbili ambapo baada ya vipimo alivyofanyiwa awali aligundulika na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news