BoT yaingia mtaani kuelimisha umma kuhusu mikopo salama

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaendesha kampeni yake ya ‘Zinduka, Usiumizwe, Kopa kwa Mandeleo’ katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo iliyoanza tarehe 30 Januari 2025, imejikita katika kuelimisha umma kuhusu ukopaji salama unaozingatia kutumia wakopeshaji wenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania, kupitia masharti na vigezo vya mkopo kabla ya kusaini na kupokea mkopo pamoja na kukopa kwa malengo ya kiuchumi na maendeleo.
Elimu kwa Umma itakayodumu kwa muda wa mwezi mmoja inafanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya sokoni, stendi za mabasi, minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi wanajitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Mikopo Salama.
Miongoni mwa maeneo ambayo yamekwishafikiwa na elimu hiyo ni Kinondoni, Magomeni, Mwananyamala, Makumbusho, kigogo, Mburahati na Mabibo na yale yanayofuata kwa siku ya kesho ni Kawe, Tegeta, Wazo, Madale.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news