SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza kuahirishwa kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) hadi Agosti 2025 baada ya Kamati ya Ufundi na Miundombinu ya CAF kushauri kwamba muda wa ziada unahitajika kwa nchi za Kenya, Tanzania na Uganda kuwa na miundombinu ambayo inaendana na viwango vya CAF ili michuano hiyo iweze kufanyika.
Taarifa ya leo Januari 14, 2025 iliyotolewa na CAF imeeleza kuwa, mafanikio mazuri yamefikiwa katika nchi waandaaji wa michuano hiyo Kenya, Tanzania na Uganda kuhusu ujenzi na uboreshaji wa viwanja, viwanja vya kufanyia mazoezi.
Vilevile hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine kwa ajili ya kuandaa michuano hiyo Kenya, Tanzania, Uganda.