DCEA yaanza mafunzo maalum ya Mtaala wa Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kulevya (UPC) kwa walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Tanga

TANGA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeanza kutoa mafunzo maalum ya Mtaala wa Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kulevya (UPC) kwa walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Tanga.
Mafunzo haya yanayohusisha walimu na waelimishaji 22 yanaendelea katika Hoteli ya Nyinda Tourist na yatahitimishwa Januari 25, 2024.
Wakati akifungua mafunzo hayo, kamishna wa Kinga na Tiba DCEA Dkt. Peter Mfisi, ameeleza kuwa mafunzo hayo ni maalumu katika kuwajengea uwezo walimu ili waweze kuwaelimisha wanafunzi kuhusu athari za dawa za kulevya kwa kutumia mbinu za kisayansi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news