DCEA yapongezwa kwa juhudi za elimu na udhibiti wa dawa za kulevya

DODOMA-Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Juliana Masabo, ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kwa juhudi zake kubwa katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria mkoani Dodoma, Mhe. Masabo alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuelimisha jamii, hasa wanafunzi, ambayo kwa sasa wako kwenye hatari ya kuingizwa kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha, Mhe. Masabo ametoa wito kwa Mamlaka kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuweka mikakati kabambe inayolenga kuelimisha na kuwakinga wananchi dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Kadhalika, alisisitiza kuwa elimu ni silaha muhimu katika kupambana na tatizo hili na kwamba ni muhimu kwa Mamlaka kuongeza nguvu katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news