DCEA yateketeza kilo 185.35 za dawa za kulevya Arusha

ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 15 Januari, 2025 imeteketeza dawa za kulevya kilogramu 185.35 katika dampo la maji ya chai liliopo wilayani Arumeru, Arusha.
Kati ya dawa zilizoteketezwa, mirungi ni kilogramu 154.35 na bangi mbichi ilikuwa kilogramu 31 ambazo ziliwahusisha jumla ya watuhumiwa watano.

Uteketezaji wa dawa hizo umefanyika mara baada ya Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kuelekeza vielelezo hivyo viteketezwe, kwani vingeweza kuleta madhara kwa binadamu endapo vitaendelea kuhifadhiwa.
Zoezi hilo la uteketezaji lilishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Arusha pamoja na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Arumeru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news