DCEA yawadaka Wapakistani, jahazi likiwa na shehena ya dawa za kulevya Bahari ya Hindi

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imesema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika operesheni zilizofanyika mwishoni mwa mwaka 2024 zilikamatwa kilogramu 673.2 za methamphetamine na heroin.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo ameyasema hayo leo Januari 9,2025 wakati akitoa taarifa za dawa za kulevya nchini mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa,mafanikio hayo yamechagizwa na juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kupambana na kudhibiti dawa za kulevya nchini kwa ustawi bora wa jamii na Taifa kwa ujumla.
Pia, Kamishna Jenerali Lyimo amesema,pamoja na ukamataji wa dawa hizo, DCEA ilijikita katika kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya na kuimarisha huduma za matibabu ya waraibu.

Amesema,kati ya dawa hizo kilogramu 448.3 zilizowahusisha raia nane wa Pakistani zilikamatwa Bahari ya Hindi zikiwa zimefichwa ndani ya jahazi lililosajiliwa nchini Pakistani kwa namba B.F.D 16548.

Kamishina Jenerali Lyimo amesema kuwa,kukamatwa kwa jahazi hilo ni mafanikio makubwa kwa mamlaka hiyo kwani iwapo kiasi cha dawa za kulevya zilzokutwa katika jahazi hilo zingefanikiwa kuingia mtaani madhara yake yangekuwa makubwa.

”Kwetu kulikamata jahazi hili ni mafanikio makubwa, limekuwa likitumika kusafirisha dawa za kulevya kwa miaka 28 sasa lakini hatimaye tumelikamata."

Vilevile Kamishna Jenerali Lyimo amesema, kilogramu 224.9 zilikamatwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi mkoani Dar es Salaam.
"Kwa mwaka 2024, jumla ya kilogramu 2,327,983.66 za dawa za kulevya zilikamatwa, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini.

"Mafanikio haya yamewezekana kwa ushirikiano wa vyombo vyote vya ulinzi, wadau wa ndani na nje ya nchi na wananchi kwa ujumla."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news