DODOMA-Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa umempitisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea urais kwa chama hicho kwa upande wa Zanzibar katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Awali akisoma hotuba ya mapendekezo hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM, ambaye pia ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amesema, rai ya wajumbe waliotoa ya kumpendekeza Rais Dkt. SSamia Suluhu Hassan na Dkt.Mwinyi kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho haipingwi kwa kuwa kila chama kina utaratibu wake.
"Kama tunataka tuamue leo kwamba Samia ndiyo mgombea wetu na Dkt.Mwinyi ndiyo mgombea wetu mamlaka hayo tunayo.
"Sasa kama tunaamua hivyo ndiyo tumeamua, sasa kinachobaki ni ushauri, wale wanajua taratibu za kisheria, taratibu za hiki, lakini watu wote watajua kwamba CCM kwenye uteuzi wa wagombea imeshamaliza."