Dorothy Semu kugombea urais 2025

DAR-Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Semu ametangaza hiyo Januari 16,2025 katika ofisi za chama hicho makao makuu Magomeni jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari.

Ameeleza kuwa, amechukua hatua hiyo akisukumwa na mambo manne ambayo ameyaona kama mapungufu na kupelekea kuwepo kwa hitaji la kupata uongozi mpya.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni, kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, changamoto ya ajira kwa vijana na udhaifu katika usimamizi wa rasilimali za Taifa.

"Nimejipima na nimeona ninatosha, nimekuwa kiongozi kwenye nafasi mbalimbali hata kabla ya kuingia kwenye siasa, pia ni kiongozi wa chama bora, chenye sera na ilani bora," amesema Semu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news