Éric Chelle aanza majukumu yake Super Eagles

ABUJA-Éric Chelle ambaye ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) ameanza majukumu yake mara moja leo Januari 13,2025.

Kocha huyo amepokelewa na kukabidhiwa rasmi majukumu ili kuanza kazi kama kocha mkuu wa timu hiyo ya Taifa baada ya Shirikisho la Soka nchini Nigeria (NFF) kumteua.
Aidha,katika mkutano wa kamati uliofanyika Januari 2,2025 mjini Abuja, Kamati Ndogo ya Ufundi na Maendeleo ya NFF ilipendekeza kuteuliwa kwa Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Mali kama Kocha Mkuu mpya wa Super Eagles.

Awali,Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 aliwahi pia kucheza timu za Martigues, Valenciennes, Lens, Istres na Chamois Niortais nchini Ufaransa.

Uteuzi wake umeanza mara moja na ana jukumu la kuiongoza Super Eagles kupata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026.Februari 2024, timu ya taifa ya Nigeria iliorodheshwa ya 28 katika viwango vya FIFA kwa ubora wa soka duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news