DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bw.Admassu Tadesse katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam leo Januari 27,2025.
Mazungumzo yao yalihusu masuala muhimu ya kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali nchini, zikiwemo sekta binafsi, nishati, kilimo, madini, na utalii.
Gavana Tutuba alibainisha kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa ajili ya kuimarisha sekta hizo, hatua inayolenga kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.