DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amefungua kikao kazi kilichoandaliwa na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Airpay Tanzania chenye lengo la kuboresha utoaji wa mikopo kwa wananchi na urejeshaji kidijitali.
Gavana Tutuba amesema urejeshaji huo wa mikopo kwa urahisi utatumia mfumo wa malipo uliotengenezwa na Airpay Tanzania ambao utaweza kutunza data na kubaini mlipaji mzuri na mbaya kwa hatua zaidi.
Aidha, Gavana Tutuba ametoa wito kwa vikundi pamoja na watu wote wanaokopa fedha serikalini na kwenye mabenki kutumia fedha hizo vizuri na kuzirejesha kwa wakati ili wengine waweze kukopa pia.