Godbless Lema kumuunga mkono Lissu na Heche uenyekiti CHADEMA

ARUSHA-Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini,Godbless Lema ametangaza rasmi kumunga mkono Tundu Lissu na John Heche katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa chama hicho Taifa.
Amesema amefanya uamuzi huo kutokana na hali ya sasa ya chama na kudai kuwa chama kinahitaji mabadiliko ya kiuongozi.

"Nimeona kwenye maswali katika mitandao ya kijamii nikuliulizwa kwamba wewe unamuunga nani mkono? Wengine wanasema Lema toa msimamo.

"Sasa leo nimekuja kutoa msimamo na mwelekeo wangu, namuunga mkono Tundu Lissu na John Heche,"amefafanua Lema wakati akizungumza na wanahabari Januari 14,2025 jijini Arusha.

Lema pia aliongeza kuwa Mbowe alimuambia mara kadhaa kwamba hatagombea tena uenyekiti lakini sasa ameonekana kugombea tena, jambo ambalo linawapa wasiwasi baadhi ya wanachama.

"Mbowe alimuambia zaidi ya mara 5 kuwa hataendelea na Uenyekiti lakini hatimaye anagombea tena," alisema Lema.

Vilevile, Lema alieleza kuwa chama hakina budi kuangalia viongozi wanaoweza kuendesha chama na kulinda demokrasia ndani yake.

"Ikifika mahali kama mtu hana pesa hawezi kuwa kiongozi wa chama hiki, hiyo ni hatari kubwa, hata huyo anayetajwa ana pesa, ana pesa za kuendesha chama?.

"Lissu siyo mropokaji, kazi yetu kama wapinzani ni kupiga kelele kwenye masuala ya msingi, kwahiyo Lissu anapiga kelele kwenye masuala ya msingi."

Lema pia alitangaza kuwa kama Freeman Mbowe hataki kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha Uenyekiti, basi atachukua msimamo madhubuti.

"Ushauri wangu kwa Mwenyekiti ni kuwa ajiondoe kwenye huu Uchaguzi, amuunge mkono Lissu. Akipigwa chini kwenye Uchaguzi atakuwa ameiaharibu vibaya sana legacy yake."

Gobbless Lema pia alitangaza kwamba hatawania tena kiti cha Ubunge wa Arusha Mjini mwaka 2025 ikiwa Mbowe atashinda uchaguzi wa Uenyekiti wa CHADEMA.

"Ninatangaza rasmi kuwa sitagombea Ubunge wa Arusha Mjini 2025 kama Mbowe atashinda uchaguzi wa uenyekiti."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news