DAR-Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed amesema watahiniwa wa shule waliopata ubora wa ufaulu katika madaraja ya 1 - III kwa mwaka 2024 ni 221,953 sawa na asilimia 42.96.
Amesema,mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja ya I-III walikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.42, hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 5.54 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Akitangaza matokeo hayo mkoani Dar es Salaam, Dkt. Said Mohammed amesema ubora wa ufaulu wa madaraja ya I-Ill ni mzuri zaidi kwa wavulana ikilinganishwa na wasichana ambapo wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 48.90 ya wavulana wote wenye matokeo na wasichana ni 102,084 sawa na asilimia 37.59 ya wasichana wote wenye matokeo.
BOFYA SHULE YAKO HAPA CHINI