Haya hapa Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2024

DAR-Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili kwa mitihani iliyofanyika Oktoba na Novemba, 2024 ambapo jumla ya wanafunzi wa shule 680,574 kati ya 796,825 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.41 wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed amesema, mwaka 2023 wanafunzi waliofaulu walikuwa 592,741 sawa na asilimia 85.31, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.10.

Aidha,kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, wasichana ni 367,457 sawa na asilimia 83.99 na wavulana ni 313,117 sawa na asilimia 8.13, hivyo wavulana wamekuwa na ufaulu bora kuliko wasichana.

Pia,wanafunzi wa kujitegemea waliofaulu upimaji na kupata sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne ni 4,205 sawa na asilimia 55.94 ambapo huu ni mwaka wa kwanza kwa wanafunzi wa kujitegemea kutahiniwa upimaji huu.Bofya hapa kwa matokeo zaidi》》》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news