DAR-Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini.
Kufuatia tathmini hiyo, Kamati ya Sera ya Fedha iliamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025.
Uamuzi huo wa Kamati wa kutobadili Riba ya Benki Kuu unalenga kuhakikisha kiwango cha ukwasi kinaendelea kuwa cha kutosha katika uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei kubaki chini ya lengo la asilimia 5, na kuwezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia takribani asilimia 5.7 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025;