Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka watanzania kuziwasilisha noti za zamani za shilingi ya Tanzania katika ofisi za BoT pamoja na benki zote za biashara na kupatiwa malipo yenye thamani ya kiasi kitakachowasilishwa katika zoezi linalotarajiwa kuanza Januari 6, 2025 hadi Aprili 5, 2025.
Zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani linahusisha shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1,000), elfu mbili (2,000), elfu tano (5,000), elfu kumi (10,000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003 pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010.