Jela kwa kuvaa nguo za JWTZ kutongozea mwanamke

MWANZA-Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu kifungo cha miezi sita, Rajabu Reli (22) ambaye ni mkazi wa wilaya hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hukumu hiyo imetolewa Januari 7, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Evodius Kisoka.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba, 2024 katika Kijiji cha Kasisa Wilaya ya Sengerema na kufikishwa mahakamani Januari 7,2025.

Rajabu alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo aliiomba Mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na kwamba alivaa sare hizo za jeshi ili zimsaidie kukubaliwa kirahisi na Mwanamke.

Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Evodius Kisoka na kumuhumu kwenda jela miezi sita ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news