DAR-Ajali ya moto iliyotokea Januari 30,2023 imeathiri jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Aidha,mamlaka hiyo imechukua uamuzi wa kuhamishia huduma zake katika jengo la Diamond Plaza, lililopo katika makutano ya Barabara ya Samora, Kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Vilevile,hatua hiyo inahusisha kuhamishia huduma za TRA kutoka ofisi yake iliyopo jengo la Mariam Tower, mtaa wa Shauri Moyo, karibu na Shule ya Uhuru jijini Dar es Salaam.