DAR-Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Dodoma Januari 18 na 19, 2025 umewateua Mwenyekiti wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza (Makamu wa Rais) wa Dk. Samia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Pia umemchagua Stephen Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
"Sisi Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) tunawapongeza viongozi hawa walioteuliwa na kuchaguliwa kwa nyadhifa hizi.
"Matumaini yetu kama Jukwaa ni kuwa viongozi hawa wataendeleza jukumu la kulitumikia taifa la Tanzania na kuwakomboa wananchi kutoka katika lindi la umaskini na kuwaletea maendeleo ya kweli.
"Tunaamini viongozi hawa watakapopata nafasi kwa maana ya kuchaguliwa wataendeleza utamaduni na jukumu la kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombovya habari bila vikwazo vya aina yoyote.
"Kama alivyosema Rais Samia kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeongezeka nchini, tunatamani nchi yetu itanue wigo wa uhuru wa vyombo vya habari wananchi wapate kila taarifa kwa wakati ziwasaidie kufanya uamuzi wakiwa na taarifa sahihi;
Tags
Chama Cha Mapinduzi
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Dr Emmanuel Nchimbi
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)