Kamati ya Bunge yaipa tano Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa namna inavyowagusa wananchi, huku ikimpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kukuza ustawi na maendeleo ya Watanzania.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatuma Toufiq, jana Januari 21, 2025, jijini Dodoma wakati ikipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali, zikiwemo usimamizi wa kazi na huduma za ukaguzi, maendeleo ya vijana, kuratibu shughuli za ajira, utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, hifadhi ya jamii, na ukuzaji wa tija. 

Ameahidi kuwa ofisi hiyo itatekeleza majukumu hayo kikamilifu ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news