DODOMA-Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko wamepokea taarifa ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka 2024/25 na Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na wizara Januari 20, 2025 viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Pia, Kamati ilipokea Taarifa ya Wizara kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yaliyotokana na Taarifa ya Mwaka ya shughuli za kamati iliyowasilishwa Bungeni mwezi Februari 2024.