Kampuni ya HAIPPA PLC yapata mapokeo chanya Mara, wanahabari washauriwa

MARA-Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC),Jacob Mugini amewataka waandishi wa habari mkoani humo kuendelea kuitangaza vyema Kampuni ya Umma ya HAIPPA PLC izidi kufahamika zaidi hapa nchini ili Watanzania wanufaike na huduma mbalimbali inazozitoa ikiwemo masoko, upatikanaji mitaji,urasimishaji na elimu ya kibiashara katika kuwasaidia kupiga hatua za kimaendeleo.
Mugini ameyasema hayo leo Januari 28, 2025, wakati akifungua semina ya mafunzo ya Uwekezaji kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mara yaliyoandaliwa na Kampuni ya Umma ya HAIPPA PLC yenye makao makuu yake Mjini Musoma ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mwembeni Complex Mjini humo huku kauli mbiu ikiwa "tuwaelimishe washiriki uwekezaji mkubwa".

Katika hotuba yake Mugini amesema kuwa, Waandishi wa Habari Mkoani humo wanalojukumu la kuzipa uzito kwa kuziandika habari za maendeleo kusudi Jamii itambue Sambamba na kazi za Wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamekuwa wakiwekeza ndani ya Mkoa huo ikiwemo Kampuni ya Umma ya HAIPPA PLC ambayo ni msaada katika kuchagiza maendeleo ya Wana-Mara na Watanzania kwa ujumla.

"Niwaombe Waandishi wa Habari, tuwe Mabalozi wa kuitangaza vyema Kampuni ya Umma ya HAIPPA PLC, imekuwa ikifanya vyema kusaidia Wananchi, wajasiriamali na pia kuchangia maendeleo kupitia Uwekezaji, mitaji, masoko, ubunifu na fursa nyingi za kiuchumi. Tuendeleeni kuitangaza kwa upana ili Watanzania iwasaidie kupata manufaa," amesema Mugini.
Aidha, Mugini amemhakikishia Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Umma ya HAIPPA PLC, kuwa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa huo itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati, huku akishukuru kutolewa kwa semina hiyo ambayo imewapa dira, na maarifa muhimu Waandishi kuandika habari za Uwekezaji kwa umahiri na ubora unaotakiwa kitaaluma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Umma ya HAIPPA PLC, Boniphace Ndengo akizungumza katika mafunzo hayo amesema kuwa, Kampuni hiyo ilianzishwa Oktoba 27, 2022, huku njozi ya kuanzishwa kwake ni kuwa akademi bora ya uwekezaji Tanzania na Afrika.

Pia, amesema dhamira ni kubuni, kujenga,kuwekeza na kuwezesha miradi mikubwa ya Afrika.

Amesema, kampuni hiyo ilianza na wanahisa. nane waanzilishi lakini mpaka sasa ina wanahisa 459, na walianza na mtaji wa Mil. 3.4, ambapo kwa sasa Wana mtaji wa zaidi ya Shilingi milioni 240. Na tangu wameanza kuuza hisa hizo Julai 2023, wameuza hisa 380,000. Huku mapokeo ya Wananchi kuhusu HAIPPA PLC akisema ni mazuri.
"Kwa nini tunahitaji elimu kuhusu uwekezaji?, Uwekezaji ni moja ya shughuli kuu tatu za kiuchumi Sambamba na ajira na Biashara.

"Kati ya Watanzania Mil. 30, watu wazima ni asilimia 0.5 ya watu 150,000, wanaoshiriki kwenye Uwekezaji mkubwa kupitia fursa za masoko ya Hisa hii ni kwa mujibu wa Taarifa za Finscope 2023.

"Kuna Wito wa Serikali kuhitaji Wawekezaji kwenye Sekta ya kilimo, Teknolojia, Miundombinu, Nishati, Madini kwani Tanzania ni moja ya nchi nyingi za Africa ambazo zina makampuni machache ya Uwekezaji. Ni vyema pia masomo ya Biashara na Uwekezaji yalipaswa kufundishwa Elimu ya Msingi na Sekondari lakini kwa Sasa hayafanyiki hivyo,"amesema Ndengo.

Ndengo amesema,kampuni hiyo inatoa huduma za ujenzi wa makampuni ya umma na makampuni ya uwekezaji, urasimishaji, uanzishaji na uendelezaji wa Biashara, ujenzi wa mitaji, huduma za masoko, ujenzi wa Miundombinu ya mifumo ya Biashara, kuelimisha na kuwezesha umma kushiriki kwenye miradi mikubwa ya Uwekezaji kupitia Kampuni za Umma na Ubia Kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Amesema,malengo ya HAIPPA PLC kwa mwaka 2025-2028 ni kutumia Teknolojia ya Mawasiliano ya Ushirikiano na Wadau mbalimbali kuwafikia wa-Tanzania Mil. 20,ili kuwapa elimu ya Uwekezaji hususan Uwekezaji kupitia Kampuni za Umma. Na kuwezesha Uanzishaji wa Kampuni za Umma angalau 50.

Pia, kuwezesha angalau Watanzania Mil. 6, kushiriki Uwekezaji mkubwa kupitia Kampuni za Umma na Miradi ya PPP. Na pia kukuza kipato cha Mtanzania (GDP per Capital) aliyemwekezaji wa HAIPPA kutoka Wastani wa Shilingi Mil. 3, kwa mwaka hadi Shilingi Mil. 30 ifikapo 2028.

Ndengo amesema kuwa, Sheria na sera zinazohimiza Uwekezaji ni pamoja na Dira ya Taifa 2020-2025 na Dira Mpya ya Taifa 2050, sera ya Uwekezaji 2022, Agenda 2030 ya Umoja wa Mataifa, Sera Mpya ya Biashara 2024, Sera ya Uwekezaji Wananchi kiuchumi 2004.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news