DAR-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyositishwa kupisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2025 na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2024).
Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, ligi hiyo sasa itaanza tena katika juma la kwanza la Februari 2025 kwa michezo ya viporo, kabla ya kuendelea na mzunguko wa 17.
Ratiba mpya na tarehe rasmi za michezo zitatangazwa hivi karibuni, ikiwapa mashabiki fursa ya kufuatilia tena ligi yao pendwa.