🔴LIVE:Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa leo Januari 19,2025

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM leo Januari 19,2025 jijini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo uliopangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 18 na 19 Januari 2025.

Kuhusu CCM

Ni chama kiongozi cha ukombozi kilichoshiriki kupigania uhuru nchi nyingi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara chenye wanachama zaidi ya milioni 12.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilianzishwa rasmi Februari 5, 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar, kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amaan Abeid Karume.

CCM imeendelea kushinda chaguzi zote sita (6) za Urais tangu kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 1992.

Huku kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinahudumia makundi yote, CCM inazo jumuiya tatu ambazo zinafanyakazi kwa kuyaunganisha makundi ya Vijana (Umoja wa Vijana wa CCM), Wanawake (Umoja wa Wanawake Tanzania- UWT) na Jumuiya ya Wazazi Tanzania.

Jumuiya hizi kila moja ina viongozi ambao muundo wake unafanana na ule wa CCM yenyewe kuanzia ngazi ya Mwenyekiti Taifa hadi ngazi za matawi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news