Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Januari 4,2025 limetangaza Matokeo ya Kidato cha Pili na Matokeo ya Mtihani wa Kujipima wa Darasa la Nne kwa mwaka 2024.
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT (SFNA) - 2024 RESULTS
Mtihani wa darasa la nne ulifanyika tarehe 23 na 24 Oktoba 2024 katika shule zote za msingi nchini Tanzania.
Vilevile la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili kwa mitihani iliyofanyika Oktoba na Novemba, 2024 ambapo jumla ya wanafunzi wa shule 680,574 kati ya 796,825 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.41 wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed amesema, mwaka 2023 wanafunzi waliofaulu walikuwa 592,741 sawa na asilimia 85.31, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.10.
Aidha,kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, wasichana ni 367,457 sawa na asilimia 83.99 na wavulana ni 313,117 sawa na asilimia 8.13, hivyo wavulana wamekuwa na ufaulu bora kuliko wasichana.
Pia,wanafunzi wa kujitegemea waliofaulu upimaji na kupata sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne ni 4,205 sawa na asilimia 55.94 ambapo huu ni mwaka wa kwanza kwa wanafunzi wa kujitegemea kutahiniwa upimaji huu.
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
FORM TWO NATIONAL ASSESSMENT (FTNA) 2024 RESULTS ENQUIRIES --- INDEX - P
CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET |