SINGIDA-Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Singida Mjini,Shwahibu Mohamed, amesema sio kweli kwamba wajumbe 29 wa mkutano mkuu kutoka Mkoa wa Singida wanamuunga mkono mgombea uenyekiti wa chama taifa Tundu Lissu.

"Mkutano tulioitiwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa tuliambiwa ni wa mashauriano lakini kwasababu akidi ya wajumbe haijatimia tumeshangaa Mwenyekiti anaita waandishi wa habari na kutoa tamko kwamba Chadema Mkoa wa Singida wanamuunga mkono mgombea uenyekiti Tundu Lissu," amesema.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo