SHINYANGA-Mkazi wa Mtaa wa Lugela katika Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama,Asha Mayenga (62) ameuawa kikatili na watu wasiojulikana kisha mwili wake kufukiwa shambani katika Kijiji cha Malindi, Kata ya Busoka alikokuwa amekwenda kupanda mpunga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi alithibitisha tukio hilo na kusema marehemu alipotea tangu Januari 13, 2025, na mwili wake ulipatikana Januari 17,2025 ukiwa na majeraha ya kupondwa kichwani.
Alisema,Polisi wanawashikilia watu watatu, akiwemo mtoto wa marehemu, kwa ajili ya upelelezi zaidi ambapo uchunguzi wa awali umebaini mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na mtoto wake, na aliwasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo