MOROGORO-Zaidi ya abiria 300,000 wamesafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) ndani ya siku 44, hivyo kufanya hadi sasa idadi ya waliopanda tangu ianze huduma kati ya Dar es Salaam na Dodoma Agosti, 2024 kufikia watu milioni 1.5.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika stesheni ya Dodoma.
Msigwa alisema takwimu hizo zinaonesha ni wastani wa abiria 300,000 kwa mwezi wanasafiri na kusisitiza kuwa, zipo treni za kutosha kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi.
Alisema vichwa vya treni 17 na mabehewa zaidi ya 78 yameingia na serikali imejipanga kutoa huduma ya vizuri kwa wananchi.
“Matatizo yanayojitokeza kwenye usafiri huu ni ya kawaida lakini pia, kuna hujuma za miundombinu tumeendelea kuchukua hatua na kuhusu umeme tatizo linalojitokeza mara moja, linatokana na shida Gridi kwenye yote ya Taifa,” alisema.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo