WAZIRI wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz ameahidi kuongeza mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ikiwa kundi la wanamgambo la Hamas litaendelea kurusha maroketi kuelekea Israel.
Katz amesema kuwa ikiwa Hamas haitaruhusu kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza, basi watakabiliwa na mashambulizi makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa muda mrefu.
Waziri Katz alitoa kauli hiyo alipokuwa akitembelea mji wa Netivot, ulio karibu kilometa 16 Mashariki mwa Palestina.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo