RUVUMA-Kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia Januari 3, 2025 Manispaa ya Songea Mjini na kuathiri kaya zaidi ya 50 Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa pole kwa waathirika hao.
Amewasihi kuwa na subira katika kipindi hichi, ambapo Serikali ikifanyia kazi athari hizo
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Mhe. Wilman Ndile, amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na wadau wengine watakaa kuona jinsi ya kuwasaidia waathirika hao.
Kata zilizo athirika na mvua hizo ni Kata ya Matogolo kaya 34 na Kata ya Seed Farm kaya 23.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo