ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paul Christian Makonda amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo kuachana na siasa za uchonganisha na badala yake ahudhurie vikao vya mipango ngazi ya halmashauri na vya ngazi ya mkoa ili kujadili pamoja kuhusu changamoto na suluhu za masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wa Arusha.RC Makonda akiambatana na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametoa kauli hiyo Januari 6,2025 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Amesema,kutohudhuria vikao hivyo na badala yake kusubiri kuwasilisha changamoto zao kwa viongozi wa kitaifa wanaofika mkoani humo kwa ziara za kikazi ni uchonganishi usiokubalika na unaokwamisha shughuli za maendeleo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo