Mama Mariam Mwinyi aendelea kurejesha tabasamu kwa Wanafunzi wa Kike, atoa wito kwa wadau

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),Mama Mariam Mwinyi amesema, wakati umefika kwa wadau kuunganisha nguvu za pamoja kuwasaidia wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zao za kielimu.
Ametoa rai kwa wadau zaidi kuunga mkono juhudi za kumaliza changamoto wanazokabiliana nazo watoto wa kike wanapokuwa skuli.
Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo katika ufunguzi wa Skuli Mpya ya Msingi Kojani Wilaya ndogo Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ameeleza kuwa, Taasisi ya ZMBF tangu mwaka 2022 imekuwa na utaratibu wa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike na tayari imewafikia wanafunzi 5,676 Unguja na Pemba.

Aidha,amesisitiza kuwa taasisi hiyo imeandaa programu mpya yenye lengo la kuwapatia wanafunzi wa kike 3,000 taulo za kike na tayari imewafikia wanafunzi 643 wa Wilaya ya Kusini na Kati Unguja.

Amefahamisha kuwa,wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakikabiliana na changomoto nyingi zinazodhorotesha kiwango chao cha elimu,utoro na kukatisha masomo hususani wanapokuwa katika ada zao za mwezi.

Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi amesema taasisi hiyo imepanga Tumaini Kit 777, soksi na viatu jozi 5,548 watapatiwa wanafunzi wa kike wa Skuli za Msingi na Sekondari za Kojani.
Hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli ya Kojani iliambatana na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa Kojani.

Ufunguzi huo wa Skuli ya Msingi Kojani ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news