Mamelodi Sundowns yawaachia alama tatu Raja Casablanca

MOROCCO-Mamelodi Sundowns imejikuta ikipanda ndege kurejea Afrika Kusini bila ushindi baada ya kuambula kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Raja Casablanca.
Wenyeji wao Raja Casablanca waliwatembezea kichapo hicho Januari 4,2024 kwenye mchezo wa raundi ya nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mtanange ambao umepigwa katika dimba la Larbi Zaouli lililopo mjini Casablanca nchini Morocco.

Bao hilo pekee liliwekwa nyavuni na Benaissa Benamar dakika ya 45' ya kipindi cha kwanza cha mtanange huo.

Aidha,timu zote zilimaliza mchezo zikiwa pungufu huku wachezaji wawili wa Mamelodi Sundowns wakioneshwa kadi nyekundu ikiwemo ya Bathusi Aubaas dakika ya 40' na Khuliso Johnson Mudau dakika ya 90'

Kwa upande wa Raja Casablanca kadi nyekundu alikula Marouane Zila dakika ya 80 ya mchezo huo.

Mbali na hayo katika Kundi B wanaoshikilia msimamo ni AS Far Rabat yenye alama nane baada ya mechi nne. Nafasi ya pili inashikiliwa na Mamelodi Sundowns yenye alama tano baada ya mechi nne.

Raja Casablanca ipo nafasi ya tatu kwa alama nne baada ya mechi nne huku Association Sportive Maniema Union (AS Maniema Union) ikiwa na alama tatu baada ya mechi nne.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news