Mapokezi ya Dkt.Mwinyi yatikisa Zanzibar,awapa neno wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu

ZANZIBAR-Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amepokewa na mamia ya wanachama wa chama hicho.
Sambamba na viongozi wakiwemo wananchi mbalimbali alipowasili Zanzibar akitokea jijini Dodoma alipoteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika hivi Karibuni.

Awali,mamia ya wananchi wa Zanzibar na wana CCM walijitokeza kwa wingi pembezoni mwa Barabara Kuu ya Uwanja wa Ndege- Kilimani kumpokea Dkt.Mwinyi aliyekuwa katika Gari la Wazi akiwapungia mkono hadi Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi alizuru kaburi la alieyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume na kuweka shada la maua pamoja na Kuzungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi na Kumpongeza pamoja na kumtakia Kila la Heri katika safari yake ya Kinyang'anyiro cha Urais wa Zanzibar.

Akizungumza na wana CCM na wananchi Uwanja wa Mapinduzi Square huko Michenzani,Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, CCM imemaliza kazi ndani ya chama ya kufanya maamuzi sahihi ya kupata wagombea wake na kazi iliyobaki ni ya kutafuta ushindi wa kishindo mwezi Oktoba katika Uchaguzi Mkuu.

Dkt.Mwinyi amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kupitia ngazi zote kwa kuthamini kazi ya Utekelezaji wa Ilani iliyofanywa naye pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuwateua tena kuwa wagombea wa chama hicho.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza wana CCM na wananchi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura litakapoanza mwezi Februari, mwaka huu na hatimaye kujitokeza kupiga kura mwezi Oktoba ili Chama Cha Mapinduzi kipate ushindi wa kishindo.

Aidha,amewasisitiza kuendelea kutunza Amani na Utulivu wa nchi hususani wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news