DAR-Wananchi mbalimbali nchini wamemtaka,Maria Sarungi kufuta kauli yake kuwa, tukio la kutekwa kwake nchini Kenya hivi karibuni linatokana na msimamo wake wa kukosoa Serikali ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi baada ya kuachiwa huru, Maria alidai kuwa watekaji wake walionesha nia ya kumvusha mpaka wa Tanzania.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam wamedai kuwa,madai ya kutekwa kwa Maria Sarungi hayana ukweli na hoja yake inalenga kupotosha umma na kuichafua Serikali katika uso wa Dunia.
"Mtu akae huko Nairobi aseme eti Serikali ya Tanzania imemteka, atekwe kwa jambo lipi mfano. Huyu, Maria Sarungi aache ujanjaujanja. Pengine fedha za kukaa Nairobi zimekata anatafuta sympathy. Watanzania tuwe tunawapuuza wapotoshaji wa aina hii,"amesema Mataro Mataro mkai wa Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Maria Sarungi amekuwa akitoa madai ya kupotosha kuhusu kutekwa kwake, akidai kuwa serikali ya Tanzania imehusika.
Lakini hakuna ushahidi wowote kuthibitisha madai haya. Kwa nini anahisi salama zaidi Kenya, nchi yenye rekodi ya uvunjaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa waandishi wa habari, na utekaji kuliko nchi karibia zote za Afrika Mashariki?.
Je, kuna uhusiano wowote kati ya Maria na serikali ya Ruto inayokumbwa na changamoto za ndani?.Ukweli wa Maria unapaswa kutiliwa shaka."
Kwa upande wake, Estomih mkazi wa Ubungo amesema,wanaharakati na wanasiasa wengi siku za karibuni wamekuwa na tabia ya kupotosha mambo ili wapate usaidizi wa kifedha ndani na nje ya nchi.
"Mifuko ya wengi imekauka, wasipotafuta kiki hawatoboi, hivyo ninamfananisha Maria Sarungi na hao wanaharakati na wanasiasa,"amesisitiza Estomih.
Hata hivyo, wanachi hao wamesisitiza kuwa,uhanaharakati nchini haupaswi kutumika kama kigezo cha kuichafua au kuipaka Serikali matope badala yake utumike kama kiunganishi na daraja la kuiwezesha Serikali kuyafikia malengo bora katika nyanja za kijamii, kiuchumi na nyinginezo.
Tags
Habari