DODOMA-Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ameahidi kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba jijini Dodoma kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuongeza kipato chao.
Mh. Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kikundi cha Twiga cha wafanyabiashara wadogo wadogo uliofanyika ndani ya Soko la Sabasaba.
“Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu yanayoendelea ndani ya Jiji la Dodoma.
"Nipo hapa leo kama Mwanachama mwenzenu wa kikundi cha Twiga ambacho tulikiasisi pamoja.
"Nina furaha kubwa kusikia mipango iliyopo ya kuongeza miradi ya kujiimarisha kiuchumi,nitajitahidi kuendelea kuwashika mkono ili muweze kusimama kiuchumi.
"Pamoja na mradi wa Shamba la mbogamboga nililowapatia,nitawaongezea na mradi wa kutoa huduma ya maji safi kwa wafanyabiashara wa soko la Sabasaba,TV ya inchi 55 kww ajili ya mradi wa kuonesha mpira na Shilingi Milioni 5 kutunisha mfuko wa Kikundi,“alisema Mavunde.