ZANZIBAR-Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mhe. Mgeni Hassan Juma amesema kumalizika kwa Kituo cha Afya Tunguu kitapunguza tatizo la kufuata huduma za afya masafa marefu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi wa Kituo cha Afya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kufuatia shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema,kituo hicho ni kituo cha kisasa na kitakuwa na ubora wa hali ya juu kutokana na kituo hicho mipango yake ipo katika daraja bora la vituo vitakavyo kuwa na huduma muhimu ikiwemo kufanya vipimo vya uchunguzi XRAY,Utrasaund kufanya upasuaji, kulaza wagonjwa na kutoa huduma nyenyinge muhimu kwa mama na mtoto.
Mheshimiwa Mgeni amewataka wananchi wa maeneo hayo pamoja na yajirani kukitumia kituo hicho mara baada ya kumaliza na kukituza ili kiweze kudumu kwa Muda mrefu na kiwe na manufaa kwa vizazi vya sasa na vya baadae.
Naye Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya, Dkt Amor Seleiman Mohamed akisoma taarif ya ya kitalam alisema jengo hilo la ghorofa moja liliaza ujenzi wake Julai 15,2023 mara tu baada ya kufanya usafi na kuvunja kituo kidogo kilichokuwepo awali na unatarajiwa kumaliza Mei 25,2025.
Alisema,kwa sasa Zanzibar ina jumla ya vituo 142 ambapo zahanati ni 90 na vituo kama hivyo 52 badala ya vile vya awali walivyonavyo 169 ambapo serikali pia itaimarisha kwa kujenga upya vituo vya afya katika wilaya zote Unguja na Pemba kwa lengo la kuwawekea karibu wananchi huduma za afya.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayuob Muhamed Mahmuod amesema katika miradi nane kati ya miradi 17 waliopanga kufungua na kuweka mawe ya msingi katika mkoa wake lakini katika sekta ya Afya mradi huo ni mradi wa tatu na huo ni mradi wa mwazo kuekewa jiwe la msingim kwa sekta ya afya.
Jumla ya shilingi bilioni 3.6 fedha za serikali ya SMZ zinatarajiwa kutumika kujenga ujenzi huo na kitahudumia watu zaidi ya 177,647 ambao ni wakazi wa Jumbi,Binguni na Tunguu na maeneo jirani na ujenzi wake umefikia asilimia 52.