KATIKA historia ya nchi yetu, mnamo Agosti 29, 2024 itatimia muongo mmoja, tangu Timu ya Serikali ya Tanzania ikwae pipa kuelekea Maputo, Msumbiji kwenye kesi ya mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Malawi.
Wajumbe wa Timu hiyo ya Serikali walikuwa 7 ambapo Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe Shamim Nyanduga alijumuika nao kutoka kushoto ni :
Hamza S. Johari (Mwanasheria),Mhe Benard Camilius Membe anbaye kwa sasa ni marehemu alimjumuisha Bw. Johari kwenye timu hii baada ya kuvutiwa sana na "Atikali Mujarab"_aliyokuwa ameiandika gazetini kuhusu mgogoro huo.
Mheshimiwa Membe ndiye alikuwa Mkuu wa msafara. Bw. Johari sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali;Mhe Patrick Luciano Tsere aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi ;
Mhe Deo Haule Filikunjombe (aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa)- Shahidi;Mhe Benard Camilius Membe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje;Mhe Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka aliyekuwa Waziri wa Ardhi;
Mhe Fredrick Mwita Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mhe John Damiano Komba (aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyasa) - Shahidi.