Michuano ya Mapinduzi Cup 2025 kuanza kesho Gombani Stadium
ZANZIBAR-Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) linatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa ya Januari 3,2025.
Michuano hiyo inaanza na Zanzibar Heroes dhidi ya Kilimanjaro Stars saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Gombani uliopo kisiwani Pemba.
Aidha,jumla ya timu nne zitashiriki mashindano hayo wakiwemo wenyeji Zanzibar, Tanzania Bara,Kenya na Burkina Faso ambapo timu mbili zitakazomaliza nafasi za juu zitakutana fainali Januari 13,2025.