DAR-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema miundombinu iliyopo ya kusambaza umeme ni ya muda mrefu na Serikali tayari imeshaanza kazi ya kuibadilisha.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akiwa katika kipindi cha dakika 45 ITV Januari 20,25.
"Miundombinu hii imekuwepo kwa miaka mingi, ndio maana tumeanza kufanya matengenezo kwa kuondoa ya zamani na kuweka mipya."
Ameongeza kuwa, kazi kubwa imefanyika kwenye kusambaza umeme Vijijini ambapo takribani asilimia 100 ya vijiji vyote vimefikiwa na nishati ya umeme.
Adha, utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hivi sasa unaelekea kwenye Vitongoji ambapo kati ya Vitongoji elfu 64 nchini Vitongoji elfu 34 vimefikiwa na nishati ya umeme.
Tags
Doto Biteko
Habari
Miundombinu ya Nishati
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Wizara ya Nishati Tanzania