Mtumishi wa TRC afikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa

KIGOMA-Januari 15, 2025 lilifunguwa shauri la jinai Na. 1337/2025 kati ya Jamhuri dhidi ya Isaka Emil Kayungu na Lusesa Peter Geoceph katika Mahakama ya Wilaya ya Uvinza mbele ya Mheshimiwa Misana Majura ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu.
Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Amrani Buyege aliieleza mahakama kuwa Oktoba 15, 2024,Bw. Isaka Emil Kayungu ambaye ni mwajiriwa wa mkataba wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kwa kushirikiana na Lusesa Peter Geoceph ambaye ni Wakala wa Huduma za Kifedha ya Mpesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Ilidaiwa, waliomba na kupokea rushwa ya shilingi 609,500 kutoka kwa mmoja wa Mfugaji Uvinza ili waweze kuziachia ng'ombe zake 65 zilizokamatwa kwa kosa la kuvuka Reli katika eneo lisiloruhusiwa kisheria.

Washtakiwa wote wawili walikana kuhusika na makosa hayo. Washtakiwa wote walikidhi masharti ya dhamana na mahakama iliwapa dhamana.

Hata hivyo,shauri limepangwa kusikilizwa tena mahakamani Februari 11, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news