DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma, tarehe 22 Januari 2025.
Majaji waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Mhe. Jaji George Mcheche Masaju, Mhe. Jaji Dkt. Ubera John Agatho, Mhe. Jaji. Dkt. Deo John Nangela, na Mhe. Jaji Latifa Alhinai Mansoor.