NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno ameambatana na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole kutoa salamu za pole kwa Familia ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mstaafu Mhe.Frederick Mwita Werema aliyefariki tarehe 30 Desemba 2024 jijini Dar es Salaam.
Naibu Mwanasheria Mkuu Serikali na Mwandishi Mkuu wa Sheria wameitembelea familia ya marehemu na kusaini kitabu cha Maombolezo tarehe 01 Januari, 2025 nyumbani kwa Marehemu Jaji Werema Mikocheni Jijiji Dar es Salaam.
Tags
Habari
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Picha
Picha Chaguo la Mhariri