MARA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ametembelea eneo alilozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na kuwataka Watanzania kutembelea eneo hilo ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na kiongozi huyo enzi za uhai wake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametembelea Kaburi la Baba wa Taifa lililoko katika Kijiji cha Mwatongo, Butiama Mkoani Mara tarehe 04 Januari, 2025 ambapo alipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na mtoto wa Baba wa Taifa, Bw. Madaraka Nyerere.
Akizungumza baada ya kutembelea nyumbani kwa hayati Mwalimu Nyerere, Mhe. Johari, amesema kufika eneo hilo ni darasa tosha la kufahamu vema historia ya nchi na Baba wa Taifa wa Taifa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameambatana na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole, na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Tags
Habari
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali