Mwinjilisti Temba aibua mazito kuelekea uchaguzi mkuu CHADEMA

DAR-Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba (Fireman) amewatahadharisha viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwataka kuachana na mihemko ya kisiasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa chama hicho.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnyukano mkali wa maneno kwenye mitandao ya kijamii kati ya kambi ya Tundu Lissu na jambi ya Freeman Mbowe kuelekea uchaguzi Mkuu wa chama hicho Januari 21,2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Lissu ambaye amejitosa kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA Taifa huku Mbowe naye akigombea kutetea nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa muda mrefu sasa,wawili hao wamekuwa na upinzani mkali uliopelekea kuwepo kwa mpasuko mkubwa wa wananchama ndani ya chama hicho.

Kufuatia hatua hiyo, Fireman amejitokeza hadharani na kuwatahadharisha wanachama wa kambi ya Lissu wanaotoa maneno ya kashfa juu ya Mbowe kuachana na mihemuko ya kisiasa kwani inaweza kusababisha chama hicho kuanguka endapo watachagua kiongozi ambaye sio sahihi kukiongoza chama hicho.

"Wenyewe wanakuja wanaongea na sisi hadharani mambo mengi nafikiri yangezungumzwa kwenye kikao hususani mambo ya kambi ya Tundu Lissu.

"Nataka niongee na wapiga kura wa Chadema kwamba mimi siwapangii wampe kura nani,nivizuri mkasoma alama za nyakati msiende kwa mihemuko,wengi wao hawajui katiba ya CHADEMA watapata shida sana kwasababu wapo kwenye mihemuko."

Mwinjilisti Temba anasema kwamba uanaharakati hautakiwi kukaa kwenye chama kwa sasa hivi,uanaharakati ni kama kudai haki,hivyo wanatakiwa kuwa wangalifu katika kuchagua Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho.

"Sasa mtu kama huyu (Mbowe) kama mmemchoka lazima mtafute njia nzuri ya kuachana na baba yenu Mbowe.

"Mimi nakuambia Lissu,kama unavyofanya staili hii ya kuchukua chama unakwenda kuabika,wewe ni mwanasiasa mshindani, nani Mwanasheria mzuri sana, unakujaje unatoa kashfa za rushwa bila ushahidi na sisi Watanzania tukaona?."

Ametoa angalizo kwa wanachama wanaomuunga mkono Lisu kama wapo kwenye mihemuko wajue mwaka mmoja au miwili chama kinaweza kuanguka, hii itakua ni kutokana na laana ya kushindwa kumheshimu Mbowe ambaye walimkuta pale amewasaidia,wakamfanyia aibu,wakamdhalilisha ili aondoke aingie Lisu,nakwamba Lisu pia ataondoka hivo hivo.

"Mimi sio CHADEMA ila nyinyi wenyewe mnakuja katuambia habari na sisi tunapima,mimi nimechekecha hizo rushwa za CHADEMA sijawahi kuziona,chaajabu Lisu akisema kitu kinakubalika,Wenje akisema kitu kinakataliwa.

"Lema ni mnafiki siku zote kakaa kimya,ndio anaibuka leo anaenda kwa Lissu anasema hivi,anaenda kwa Mbowe anasema hivi,ana panga hivi hawa wakina Lema ndo walikua TLP, na Lema amepata heshima Arusha kutokana na Mbowe.

Fireman ameongeza kuwa hakuna anaepinga kama Lowasa alopohamia CHADEMA zaidi ya wabunge 70 walipatikana,Lowasa amerudisha fomu pale katikati ya jiji mitaa yote watu wanatembea barabara nzima,mikutano yake kila mahali watu wamejaa,leo Lisu anakuja anaanza kumkosoa Lowasa.

"Shida ya Mbowe sio haya yanayozungumzwa,shida ya Mbowe ni kukikataa kikundi cha baadhi ya Watanzania wachache waishio nje ya nchi( Diaspora) walivyokua wanataka kuleta kesi zao kuanza kuipinga serikali kusimama kwenye majukwaa kwa ajili ya wao kupata uraia pacha.

"Ile Mbowe akasema hatuwezi kukubali,hawa watu waje kwenye chama hivi ni vikundi vya huko nje viingie kwenye chama vituamulie ndipo wakagawanyika wakamchukia Mbowe,walipoanzisha kesi kuitaka serikali ilazimishwe mahakama kuu iingilie kati na ille kesi ikatupwa kwasababu Mbowe hakuhusika wakaapa kwamba,kuhakikisha lazima Mbowe atoke kwenye chama hicho.

"Ndio maana wakamtumia Dkt.Slaa,Lissu pamoja na Lema wakusanye fedha kwa ajili ya mchakato wa kumng'oa Mbowe,hivyo Lema alipoenda Canada juzi alienda kuchukua fedha ndio maana Lema alituambia anamkusanyia Lisu fedha za kampeni,sasa wanamkusanyia fedha za nini kama Lisu hatoi rushwa?."

Kwa mujibu wa Fireman amesema kuwa,wapo Watanzania waliopo nje ya nchi wanatoa rushwa huko mikoani kuwatafuta Vijana na kuwavisha nguo za CHADEMA ili wamtukane Mbowe.

Hata hivyo, amemaliza kwa kuwaasa wapiga kura wa Chadema wampende Lissu,wampende Mbowe kwani atakayeshinda kati yao ni wa kwao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news