Naibu Waziri Londo aongoza ujumbe muhimu Kampala

KAMPALA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia, Masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis L. Londo (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Kilimo, Maji, Mazingira na Maendeleo Vijijini na Mawaziri wa Mambo ya Nje uliofanyika jijini Kampala, Uganda tarehe 10 Januari, 2025.
Mkutano huo wa awali ambao ulikutanisha Mawaziri na Wakuu wa Taasisi Mbalimbali za Kimataifa kutoka barani Afrika umefanyika kabla ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Mpango Madhubuti wa Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP).
Mkutano huo umejadili masuala anuai juu ya upitishaii wa Azimio la Kampala kuhusu Mifumo Madhubuti na Endelevu ya Kilimo na Chakula barani Afrika (Kampala CAADP Declaration on Building Resilient and Sustainable Agrifood Systems in Afrika) ambalo madhumuni yake ni kubadili mfumo wa awali uliojikita kwenye kilimo pekee na kwenda kwenye Mifumo ya Kilimo Chakula (Agrifood).

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wengine wa Sekta Mbalimbali ikiwemo Mhe.Hussein M. Bashe (Mb.); Waziri wa Kilimo, Mhe. Juma H. Aweso (Mb.), Waziri wa Maji, Mhe. Shamata S. Khamis (Mb.), Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar na Mhe. Alexander P. Mnyeti (Mb.) Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news