DAR-Ndoa ya mwigizaji Jackline Massawe (Wolper) na mume wake Rich Mitindo haina uhai tena, ni baada ya Wolper kutangaza kuachana rasmi na mume wake.
Wolper na Rich Mitindo walifunga ndoa hiyo Novemba,2022 katika Kanisa la St. Peter’s lililopo jijini Dar es Salaam.
Nyota huyo wa filamu nchini ametangaza kuachana na Rich Mitindo (Baba P) kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kutaka talaka.
“Mimi na mzazi mwenzangu Rich (Baba P) hatupo pamoja (TUMEACHANA). Nipo kwenye process za Divorce/Talaka. Hivyo, mashauri yote na huruma juu ya mambo yanayoendelea na mzazi mwenzangu, msiyalete kwangu tena. Ni mtu ambae yupo huru kufanya chochote kinachompendeza.”
Wawili hao baada ya kufunga ndoa yao miaka miwili iliyopita wamebarikiwa kupata mtoto mmoja