Ni Mbowe au Lissu?

DAR-Leo Januari 21,2025 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya uchaguzi wa viongozi wake wa ngazi ya taifa huku nafasi ya Mwenyekiti wa chama ikiwaniwa na watu watatu.
Mosi ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Freeman Mbowe, Makamu mwenyekiti Tundu Lissu na Odero Charles Odero. Hata hivyo mchuano umekuwa mkali zaidi kati ya Lissu na Mbowe.

Mchuano huo wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu, aliyewahi kuwa Mbunge wa CHADEMA katika Jimbo la Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), umeibua mambo mengi.

Wababe hawa wawili katika siasa za chama hicho wanaitaka nafasi ya uenyekiti ambayo ni ngazi ya juu zaidi katika chama hicho.Ni Mbowe au Lissu, majibu watakuwa nayo wapiga kura leo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news