DAR-Shirika la Ndege la Precision Air limetangaza kuanzishwa kwa huduma mpya ya usafiri wa ndege kwenda Iringa kuanzia Machi 3,2025.
Safari hizo zitafanyika kila Jumatatu, Jumatano, na Ijumaa, zikiwaunganisha abiria kati ya Dar es Salaam, Iringa, Dodoma, na kwingineko kupitia mtandao wa Precision Air na
washirika wake.
Safari hii mpya ni sehemu ya juhudi za Precision Air za kuendelea kuimarisha upatikananji wa huduma za usafiri wa anga nchini, ili kusaidia ukuaji wa kiuchumi, kwa kutoa huduma za usafiri wa anga za uhakika na nafuu kwa jamii kote Tanzania.
Kuanzishwa kwa safari za ndege kati ya Dar - Iringa kutapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa safari na kuwapa abiria usafiri wa anga ulio nafuu.